emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

ASANTE KWA KUJIUNGA NA NSSF





Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, amempongeza na kumkabidhi Joyce Sungura, kadi ya uanachama wa NSSF baada ya kujiunga wakati alipotembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. NSSF inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima, wavuvu, wafugaji, wachimba wadogo wa madini, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote ambao wanapofika katika banda hilo watapewa elimu na kuandikishwa kuwa wanachama wachangiaji.