emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

Frequently Asked Questions

1.1. NSSF Taarifa - Mobile App

Kwa kutumia programu hii utapata taarifa za michango, salio na huduma mbalimbali.

Jinsi ya Kutumia:

• Pakua "NSSF Taarifa" kutoka "Google Play Store".

• Utapata taarifa binafsi za uanachama.

• Kuangalia taarifa za michango iliyowasilishwa kwenye Shirika bofya "Statements".

1.2. NSSF Taarifa - WhatsApp

Jinsi ya Kutumia:

• Hifadhi namba maalum ya 0756 140 140 kwenye simu.

• Fungua Programu ya WhatsApp kisha tuma ujumbe wa salamu "Hello" au "Habari".

• Utapokea ujumbe wenye maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii.

• Andika neno "Statement" kupata taarifa ya michango yote iliyowasilishwa, au tuma neno "Balance" kupata ujumbe wenye salio la michango iliyowasilishwa.

1.3. NSSF Taarifa - SMS

Jinsi ya Kutumia:

Ingia ingia kwenye programu ya Ujumbe Mfupi (SMS) kisha tuma ujumbe kwenda namba 15200 kupata huduma zifuatazo:

Kwa Salio/Balance ya michango tuma ujumbe

NSSF SALIO (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF BALANCE (Member Number) (Year)

Kwa Taarifa/Statement ya michango tuma ujumbe

NSSF TAARIFA (Namba ya Mwanachama) (Mwaka)

Au

NSSF STATEMENT (Member Number) (Year)

1.4. Mfumo wa ‘Member Portal’

Kupitia Mfumo ambao unapatikana katika tovuti ya Shirika yaan www.nssf.go.tz utaweza:

• Kuangalia taarifa za michango yote iliyowasilishwa na Mwajiri wako katika Shirika au michango iliyowasilishwa na mwanachama kwa wanachama wa hiari.

• kupata taarifa za michango (Statements).

Ili upate kuona taarifa zako unatakiwa kuwa namba ya simu ambayo uliisajili NSSF endapo ulibadilisha au haukuiweka tunaomba ufike katika ofisi ya

NSSF iliyojirani yako ili kuweza kuboresha Taarifa zako na kuendelea kufurahia huduma zetu

“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”

Kama kwa namna yoyote umegundua kwamba mwajiri wako hawasilishi michango yako NSSF na hali unakatwa asilimia kumi (10%) kutoka katika mshahara wako tafadhali fanya yafuatayo:

•Tunaomba kwa kupitia ukurasa huu utupatie taarifa muhimu inbox kama jina la mwajiri, namba yako ya uanachama, mkoa mwajiri alipo, tarehe ya kuanza kazi na namba yako ya simu ili tuweze kushughulikia suala hili na kulitatua.

•Kufikisha suala hili kwenye ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe na kuonana na Afisa Matekelezo.

•Kuwasilisha lalamiko lako kupitia kwenye dawadi la malalamiko ambalo lipo kwenye kila ofisi ya NSSF

Tanzania nzima au kwa kutumia barua pepe: customercare@nssf.go.tz au simu bure 0800116773 ambapo suala lako litafanyiwa kazi.

NB: Pamoja na hivyo NSSF tunawajibika kufutilia michango kwa mwajiri ili aweze kumuwekea mwanachama kwa wakati

Ili
mwanachama wa NSSF aweze kubadili majina ambayo yamekosewa/ yametofautiana
katika usajili anatakiwa azingatie yafuatayo:





i)
Ili kuweza kubadili majina unatakiwa kwenda kwa mwanasheria ambaye atakuandalia
kiapo cha kubadili majina "Deed Poll".



AU



Unaweza
kwenda mahakamani na kuandaliwa kiapo cha kubadili majina " Deed
Poll".





ii)Utawasilisha
kiapo cha kubadili "Deed poll" Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi au Ofisi za Aridhi Mkoa na
Kanda kwa Msajili wa Hati "Registrar of Titles" kwa ajili ya malipo
ya usajili.





iii)
Baada ya kukamilisha hatua ya pili, utakuja kuwasilisha katika ofisi za NSSF(Mkoa
husika) ukiwa na kiapo cha kubadili majina "Deed poll"
kilichosajiliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi( Hatua hii
haitahusisha malipo yoyote).





iv)
Endapo jina lilikosewa na NSSF wakati wa usajili, mwanachama atafika katika
ofisi ya NSSF na kubadili jina hilo bila malipo.





Angalizo:
Ili kupata kadi mpya utalipia TZS. 5000/= ambayo italipwa kupitia namba ya
malipo ya Serikali utakayopewa.

Ili kuweza kupata huduma ya matibabu tunaomba uzingatie yafuatayo yafuatayo:

• Huduma ya matibabu ya NSSF inatolewa kwa mwanachama ambaye amesajiliwa chini ya huduma hiyo

ambapo atatibiwa katika hospitali moja kati ya hospital ambazo zimeingia mkataba na NSSF.

• Mwanachama awe amechangia angalau michango ya miezi mitatu mfululizo karibu na kupata huduma ya kupata matibabu

Kama vigezo hivyo vimezingatiwa na huduma haikuweza kupatikana basi tunaomba utupatie taarifa

muhimu kama vile jina la mwajiri, namba yako ya uanachama, majina kamili, mkoa mwajiri alipo, tarehe ya kuanza kazi na namba yako ya simu ili tuweze kushughulikia zaidi.

Pia Unaweza kufika kwenye ofisi ya NSSF iliyopo karibu nawe ili waweze kutatua tatizo lako.

Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama wa NSSF aliyepoteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira yake imefika ukomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (resignation).

Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama mwenye sifa zifuatazo

Mwanachama awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na nane (18)

Awe mwanachama wa NSSF aliye poteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira imefikia kikomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation)

Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Asiwe na sifa ya kulipwa mafao ya muda mrefu ambayo ni Pensheni ya uzee, Ulemavu au urithi/wategemezi

Ithibitishwe kuwa mwanachama hayupo kwenye ajira yoyote Awe na umri chini ya miaka 55.

Mwanachama atalipwa asilimia 33.3 ya mshahara wake aliokuwa anapata wakati akiondoka kwenye ajira. Malipo hayo yatalipwa kwa kila mwezi mfululizo kwa kipindi kisichozidi miezi sita ndani ya mwaka mmoja. Malipo ya kila mwezi yatakoma iwapo mwanachama atapata ajira Mwanachama ambaye atakuwa hajatimiza michango ya miezi 18 atalipwa mkupuo wa asilimia hamsini (50%) ya jumla ya michango yake

Iwapo mwanachama ataendelea kukosa ajira baada ya kuisha kwa kipindi cha miezi 18, anaweza kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi Mkuu ili baki ya michango yake ihamishiwe kwenye mpango wa uchangiaji wa hiari atakaouchagua mwenyewe ili aendelee kuchangia kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mpango husika.

Tahadhari:Ni kosa la jinai chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018, kwa mtu yeyote kwa makusudi kutoa taarifa za uongo/ zisizo sahihi kwa lengo la kujipatia mafao yeye mwenyewe au mtu mwingine.

Ili kuweza kupata huduma ya matibabu zingatia yafuatayo:

• Huduma ya matibabu ya NSSF inatolewa kwa mwanachama ambaye amesajiliwa chini ya huduma hiyo ambapo atatibiwa katika hospitali moja kati ya hospitali ambazo zimeingia mkataba na NSSF.

• Mwanachama awe amechangia angalau michango ya miezi mitatu mfululizo karibu na kupata huduma ya kupata matibabu Kama vigezo hivyo vimezingatiwa na huduma haikuweza kupatikana basi tunaomba utupatie taarifa muhimu kama vile jina la mwajiri, namba yako ya uanachama, majina kamili, mkoa mwajiri alipo, tarehe ya kuanza kazi na namba yako ya simu ili tuweze kushuhulikia Zaidi.

Pia Unaweza kufika kwenye ofisi ya NSSF iliyopo karibu nawe ili tuweze kutatua tatizo lako.