emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

Frequently Asked Questions

Inachukua mwezi mmoja mpaka mwanachama kupata mafao yake endapo taratibu zote zimezingatiwa ikiwemo uwasilishwaji wa michango ya mwanachama kwa kwa wakati, pia ili mwanachama apate kufungua madai yake anatakiwa akae mwezi mmoja na atatakiwa kufikia katika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ukiwa na barua yako inayoonesha kuachishwa kazi au Barua ya kustaafu/ulemavu ili kupewa nyaraka nyingine zinazotakiwa.

Kwa Madai mengine kama mirathi, ujauzito, matibabu na msaada wa mazishi tafadhali fika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu nawe kwa msaada zaidi.

“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”

Kama kwa namna yoyote umegundua kwamba mwajiri wako hawasilishi michango yako NSSF na hali kua unakatwa asilimia 10% kutoka

katika mshahara wako tafadhali fanya yafuatayo:

• Tunaomba kwa kupitia ukurasa huu utupatie taarifa muhimu inbox kama jina la mwajiri, namba yako ya uanachama, mkoa

mwajiri alipo, tarehe ya kuanza kazi na namba yako ya simu ili tuweze kushuhulikia suala hili na kulitatua.

• Kufikisha suala hili kwenye ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe na kuonana na afisa matekelezo.

• Kuwasilisha lalamiko lako kupitia kwenye dawadi la malalamiko ambalo lipo kwenye kila offisi ya NSSF

Tanzania nzima au kwa kutumia barua pepe: customercare@nssf.go.tz au simu bure 0800116773 ambapo suala lako litafanyiwa kazi.