emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

NSSF Schemes

Hifadhi Scheme

SKIMU YA TAIFA YA HIFADHI YA JAMII KWA WANANCHI WALIOJIAJIRI

UTANGULIZI

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hutoa huduma za Hifadhi ya Jamii kwa wanachama walioajiriwa kwenye Sekta Binafsi na waliojiajiri.

Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliojiajiri (National Social Security Scheme for Self Employed - Hifadhi Scheme) imeanzishwa kwa ajili ya kuhudumia Wananchi waliojiajiri kwenye shughuli za kiuchumi.

SKIMU

  • Kuongeza wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa makundi ambayo hayanufaiki na huduma hizi ingawa wanashiriki kikamilifu kuchangia uchumi wa Nchi
  • Kusaidia juhudi za Serikali za kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi
  • Kuongeza nguvu za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Nchi
  • Kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla

WALENGWA WA SKIMU

Wananchi waliojiajiri katika maeneo mbalimbali kama;

  • Kilimo
  • Ufugaji
  • Uvuvi
  • Uchimbaji mdogo wa madini
  • Sanaa mbalimbali
  • Bodaboda
  • Machinga
  • Biashara nyingine ndogo ndogo

(wasusi, wachuuzi masokoni, mama lishe/baba lishe n.k)

  • Wananchi waliojiajiri katika makundi yanayofanya kazi kwa vipindi maalum

SIFA ZA KUJIUNGA

Kujiandikisha katika Skimu hii, mwanachama anapaswa awe na sifa zifuatazo;

  • Umri wa kuanzia miaka 15 hadi 70
  • Asiwe ni mnufaika wa mafao ya Pensheni kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini Awe ni Mtanzania na mkazi wa Tanzania Bara

TARATIBU ZA KUJIUNGA

Kujiandikisha katika Skimu hii, mwanachama anapaswa atimize yafuatayo;

  • Kujaza fomu ya uandikishaji kwa kuweka taarifa binafsi
  • Kuwasilisha namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Leseni ya udereva au kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kuwasilisha fomu kwa njia ya mtandao au kufika kwenye ofisi za Mfuko

MICHANGO

  • Mwanachama anapaswa kuchangia kuanzia 30,000 au 52,200 au zaidi kwa mwezi
  • Mwanachama anaweza kuchangia kidogo kidogo kwa siku, wiki, mwezi, muhula au msimu
  • Mwanachama anapaswa kutumia namba ya kumbukumbu ya malipo (control number) kuwasilisha michango

NJIA ZA UCHANGIAJI

  • Simu ya kiganjani kupitia mitandao ya simu (ARAFA-USSD) *152*00#
  • Benki au wakala wa benki
  • Lango la Huduma za NSSF (NSSF Portal) kupitia tovuti (www.nssf.go.tz)

MAFAO

Skimu hii inatoa mafao yafuatayo;

  • Mafao ya Pensheni ya Uzee
  • Mafao ya Urithi
  • Mafao ya Ulemavu
  • Mafao ya Uzazi
  • Mafao ya Matibabu
  • Mafao ya kujitoa (kuchukua sehemu ya michango au kuchukua michango yote)
  • Mafao ya Msaada wa Mazishi

Huduma za kidijitali (ARAFA-USSD) *152*00#

  • Mwanachama anaweza kujisajili, kulipia michango na kuhakiki michango/ kuangalia salio
uchaguzi