emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF ilivyoshiriki Maonesho ya Nanenane 2025 – Kitaifa Dodoma



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulishiriki katika Maonesho ya Nanenane 2025, ambayo kitaifa yalifanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NSSF ilishiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo kuhusu mafao, uandikishaji wa wanachama wapya, hususan kutoka sekta binafsi na kwa wananchi waliojiajiri, njia rahisi za kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za kidigitali, ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya kupambana na vitendo vya rushwa.