emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF Yashiriki Maonesho ya Nanenane 2025 na Kutwaa Tuzo – Lindi




Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki katika Maonesho ya Nanenane 2025 yaliyofanyika katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo mkoa wa Lindi ambako uliibuka mshindi wa pili katika kipengele cha Kampuni za Fedha na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Kupitia ushiriki wake, NSSF ilitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii, ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu mafao yatolewayo na Mfuko, uandikishaji wa wanachama wapya, hususan kutoka sekta binafsi na kwa wananchi waliojiajiri, njia rahisi za kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za kidigitali, ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya kupambana na vitendo vya rushwa.