emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF Yashiriki Maonesho ya Nanenane 2025 – Kagera


NSSF Yashiriki Maonesho ya Nanenane 2025 – Kagera

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki katika Maonesho ya Nanenane 2025 yaliyofanyika katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Kagera, chini ya kaulimbiu: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."

Kupitia ushiriki wake, NSSF ilitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii, ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu mafao yatolewayo na Mfuko, uandikishaji wa wanachama wapya, hususan kutoka sekta binafsi na kwa wananchi waliojiajiri, njia rahisi za kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za kidigitali, ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya kupambana na vitendo vya rushwa.