emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA YA MAONESHO YA 'TANZANIA SAMIA CONNECT ARUSHA’ KWA KUJIUNGA NA NSSF



Na Mwandishi Wetu Arusha

Wananchi mkoani Arusha wametumia fursa ya maonesho ya ‘Tanzania Samia Connect’ kwa kupata elimu ya hifadhi ya jamii na kuweza kujiunga pamoja na kuchangia katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Wananchi hao ambao wengi wao wamejiajiri kupitia sekta ya kilimo, ufugaji, uvuvi, madini (wachimbaji wadogo wadogo), usafirishaji (boda boda na bajaji), sekta ya biashara ndogo ndogo (Machinga, Mama/Baba lishe, ususi, muuza mkaa, muuza nyanya na wajasiriamali wengine wote) wamepata elimu hiyo ya hifadhi ya jamii hususan ‘Hifadhi Scheme’ ambayo inatoa nafasi kwa wananchi waliojiajiri kupata kinga katika maisha ya uzeeni au pindi majanga yanapotokea ambapo NSSF inakuhakikishia inalinda kesho yako kwa kutoa huduma na mafao mbalimbali yakiwemo mafao ya matibabu.

Aidha, NSSF imeweka mifumo rafiki ya kidijitali ya Arafa kwa ajili ya kuchangia na kujiunga kupitia *152*00# ambapo mwanachama anaweza kuchangia kuanzia shilingi elfu thelathini (30,000/-) kila mwezi ili kunufaika na Mafao ya Uzeeni na hata Mafao ya Matibabu kwa mwanachama; au Shilingi elfu hamsini na mbili na mia mbili(52,200/) kwa kutoa kidogo kidogo kwa siku, wiki, mwezi au msimu kulingana na kipato chake ili kunufaika na Mafao ya Uzeeni na mafao mbalimbalj yakiwemo Mafao ya Matibabu kwa mwanachama na wategemezi wake