Frequently Asked Questions
Ili kuweza kubadili majina yako unatakiwa kwenda kuapa mahakamani, kisha kusajili ardhi (vizazi na vifo) baada ya hapo utakuja na viambata vyote kubadili jina lako katika ofisi yoyote ya NSSF bure, lakini ili kupata kadi mpya utalipia TZS 5000 ambayo italipwa kupitia namba ya malipo ya Serikali utakayopewa
Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi.
Ili kupata kitambulisho chako unatakiwa kufika katika ofisi ya NSSF ambapo uandikishaji ulifanyika au fika ofisi yoyote ya NSSF iliyopo karibu nawe kwa msaada Zaidi.
“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”
Ili upate kuona taarifa zako unatakiwa kuwa namba ya simu ambayo uliisajili NSSF kwa mara ya kwanza, endapo umebadilisha au haukuiweka kabisa au endapo majina majina yamebadilika tunaomba ufike katika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kuweza kuboresha Taarifa zako na kuendelea kufurahia huduma zetu
Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa na NSSF. Tafadhali fika ofisi za NSSF kwa maelekezo zaidi.
Ili kujiunga na uanachama utatakiwa kuwa na namba au kitambulisho cha taifa (NIDA) na kufika kwenye ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe.
Au
kama hauna kitambulisho cha Taifa fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako na utaweza kuandikishwa.
Baada ya kujiunga kuwa mwanachama utatakiwa kufikisha namba ya uanachama kwa mwajiri wako kama umeajiriwa
au kujichangia kiasi cha kuanzia shilingi 20,000.00 au zaidi kila mwezi kwa mwanachama wa hiari.
NB:NSSF inaandikisha wanachama kutoka katika makundi yafuatayo:
• Wafanyakazi walioajiriwa katika sekta binafsi
• Raia wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania Bara
• Watumishi wa taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara
• Watu waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi
“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”
Ili kupata kitambulisho chako unatakiwa kufika katika ofisi ya NSSF ambapo uandikishaji wa awali ulifanyika au fika ofisi yoyote ya NSSF iliyopo karibu nawe kwa msaada zaidi.
“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”
Ili uweze kupata huduma ya matibabu itakupasa kufika ofisi ya NSSF uweze kusajiliwa kwenye huduma ya matibabu ambapo unatakiwa kuwa na michango ya miezi mitatu iliyolipwa karibu na kipindi cha kupata huduma ya matibabu. Baada ya kuingizwa kwenye mfumo wa matibabu utatumia kadi yako ya NSSF katika hospitali utakayochagua ambayo imeingia mkataba na NSSF
“NSSF Tunajenga Maisha yako ya Sasa na Baadaye”