News
Kamati ya Bunge ya Kudumu PIC watembelea Daraja la Nyerere Kigamboni

Kamati ya Bunge ya Kudumu PIC watembelea Daraja la Nyerere Kigamboni
Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Vumma Augustine, wametembelea na kukagua mradi wa Daraja la Nyerere, Kigamboni unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo NSSF, ambapo katika mradi huo walijionea namna Mfuko unavyotekeleza moja ya jukumu lake la uwekezaji.