emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​MAKAMU WA RAIS ALIPOFUNGUA MASHINDANO YA SHIMMUTA 2022, MKOANI TANGA*NSSF ni mojawapo ya Taasisi za Serikali 52 zinazoshiriki mashindano hayo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amefungua Mashindano ya Michezo kwa Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) kwa mwaka 2022 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

NSSF ni miongoni mwa Taasisi 52 zinazoshiriki mashindano ya SHIMMUTA kwa mwaka huu yaliyoanza tarehe 15 Novemba, 2022 jijini Tanga huku taasisi hizo zikichuana katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na michezo ya jadi.

Akizungumza wakati wa hotuba yake kwenye ufunguzi huo Mhe. Dkt. Isdor Mpango amezipongeza taasisi zinazoshiriki na kuzitaka taasisi nyingine zijitokeze kushiriki kwani michezo huleta mshikamano mahali pa kazi na pia hudumisha udugu baina ya taasisi. Amewaasa washiriki kuzingatia kanuni na taratibu zote za kazi kwani wako katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Mashindano hayo yanaongozwa na Kauli mbiu hii: “Michezo ni fursa, tuitumie vyema kuimarisha afya za

wafanyakazi kwa uchumi imara wa Taifa.”

NSSF pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao mbalimbali, vilevile inashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo ili kuimarisha afya za wafanyakazi mahala pa kazi.