News
MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA NSSF, ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NSSF

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Bi. Mwamini Malemi, ametembelea Makao Makuu ya NSSF jijini Dar es Salaam, leo tarehe 5 Disemba 2023, na kuzungumza na Menejimenti ya Mfuko, ambapo amepata nafasi ya kupokea taarifa ya utendaji kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, ambaye alitumia fursa hiyo pia kumpongeza na kuahidi kumpatia ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na Bodi ya Wadhamini kwa ujumla.