News
NAIBU WAZIRI KATAMBI ATEMBELEA BANDA LA NSSF NANENANE
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobasi Katambi, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), na kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima 'Nane Nane' yaliyofanyika Mkoani Dodoma. Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara Mifumo Endelevu ya Chakula”
NSSF inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, elimu kuhusu huduma za NSSF kidijitali, elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Uwekezaji na elimu kuhusu mafao yanayotolewa na NSSF

