emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA NANENANE 2025 – TABORA



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaendelea kutoa huduma katika Maonesho ya Nanenane 2025 yanayoendelea katika mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora chini ya kaulimbiu: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."

NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, elimu kuhusu kujichangia kupitia simu ya kiganganjani popote walipo, pia kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za Mifumo mbalimbali ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa.