emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YANG’ARA KITAIFA KATIKA USALAMA MAHALA PA KAZI – YASHINDA TUZO KUTOKA OSHA



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepata tuzo ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha Kuboresha Usalama Maeneo ya Kazi ya Wananchi (Umma), tuzo ambayo imetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) tarehe 29 Aprili, 2025 katika ukumbi wa Bishop Rwoma, Mkoani Singida.

Tuzo hiyo imepatikana chini ya kundi la Utawala wa Umma na Ulinzi; Usalama wa Jamii kwa Mujibu wa Sheria, ikiwa ni uthibitisho wa jitihada madhubuti zinazofanywa na NSSF katika kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama na yenye afya kwa wafanyakazi wake.

Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo alikuwa Mhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Bi. Lulu Mengele, ameushukuru uongozi wa NSSF kwa kuweka mazingira bora ya kazi kwa kuzingatia viwango vya usalama na afya mahala pa kazi, hali ambayo imeongeza tija kwa wafanyakazi na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wanachama.

Bi. Lulu aliongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya dhamira ya dhati ya Mfuko katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao stahiki kwa wanachama.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidigitali Katika Kuimarisha Usalama na Afya Mahala pa Kazi"