emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF YAPATA USHINDI DHIDI YA TRA


MICHEZO YA SHIMMUTA MKOANI TANGA

* NSSF YAPATA USHINDI DHIDI YA TRA

Timu ya mpira wa Kikapu (Basketball) ya NSSF imepata ushindi wa seti 39 kwa 26 dhidi ya timu ya mpira wa Kikapu ya TRA. Mashindano ya SHIMMUTA yanaendelea mkoani Tanga ambapo mchezo huo umefanyika katika viwanja vya Mkwakwani leo jioni, tarehe 17 Novemba 2022.

NSSF pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao mbalimbali, vilevile inashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo ili kuimarisha afya za wafanyakazi mahala pa kazi.