emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF yarudisha kwa jamii na kusaidia vifaa vya kuboresha huduma za afya

Na MWANDISHI WETU,Kilimanjaro. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kutekeleza jukumu lake lingine la kurudisha kwa jamii kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mazingira ya utoaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Kituri, Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.Baadhi ya vifaa hivyo ni meza, viti, makabati na mabenchi kwa ajili ya wagonjwa ambapo NSSF kupitia sera yake ya uchangiaji na udhamini (CSR), imekuwa ikiiunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maeneo ya afya, elimu, michezo na maeneo mengine ya kijamii kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania kwa ujumla. NSSF imekuwa ikifanya hivyo kwa kurudisha kwenye jamii kupitia sekta ya afya, elimu pamoja na huduma za kijamii.Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja wa NSSF Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Audrey Claudius amemkabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kituri Mhe. Athuman Ramadhan Karavile, kwa ajili ya Zahanati hiyo ya Kituri.Msaada huo umetolewa mwishoni mwa wiki hii huko Mwanga, mkoani Kilimanjaro.