News
NSSF YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KWA WAJASIRIAMALI SOKO LA MWANANYAMALA NA MANZESE

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasirimali na wafanyabiashara waliopo soko la Mwananyamala na Manzese, Dar es Salaam.
Kupitia utoaji huo wa elimu ya hifadhi ya jamii, NSSF inaandikisha wanachama wapya na kuhamasisha uchangiaji ambapo hamasa ya wajasiriamali kupata elimu na kujiunga imekuwa kubwa.