News
NSSF YATOA TUZO KWA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOWASILISHA MICHANGO KWA WAKATI
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba amekabidhi tuzo kwa baadhi ya vyombo vya habari vinavyowasilisha michango kwa wakati, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa unaotolewa na vyombo vya habari kwa wafanyakazi wao. Vyombo vilivyokabidhiwa tuzo hizo ni Independent Television Limited, Azam Media Limited, Mwananchi Communications Limited na Jamhuri Media Limited katika Mkutano wa NSSF na Jukwaa la Wahariri wa Tanzania (TEF), tarehe 1 Oktoba 2024, katika ukumbi wa Mafao House Ilala Dar es Salaam.