emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF YATWAA TUZO YA USHINDI





Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetwaa Tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NSSF imepokea cheti na tuzo hiyo kwa kutambua utendaji kazi wa hali ya juu katika Wiki ya Huduma za Fedha inayomalizika leo.



Wiki ya huduma za fedha hufanyika kila mwaka na inaratibiwa na Wizara ya Fedha ikishirikisha wadau wa masuala ya fedha nchini, ambao ni wizara na taasisi za serikali, mabenki, makampuni ya bima pamoja na wadau wengine wa serikali na sekta binafsi.



Kwa mwaka huu, Wiki ya Huduma za Fedha imefanyika jijini Arusha na ilianza tarehe 20 na inafikia tamati tarehe 26 Novemba 2023.