emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF YAWATAKA TWCC KUCHANGAMKIA FURSA YA KUJIUNGA NA KUJIWEKEA AKIBAMeneja wa Sekta isiyo rasmi wa NSSF, Bi. Rehema Chuma akiwa na wafanyakazi wengine wa NSSF, wametembelea banda la Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama wa Chemba hiyo wanaoshiriki Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), ambapo aliwaeleza umuhimu wa kujiwekea akiba kwa kujiunga na kuchangia NSSF ambapo kwa mwezi watachangia kiasi cha shilingi 30,000 kima cha Chini.