emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​WATEJA WA NSSF KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA KIDIJITALI


WATEJA WA NSSF KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA KIDIJITALI

Na MWANDISHI WETU,
Dar es Salaam. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ofisi ya Makao Makuu umezindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli mbiu isemayo "Huduma Bora Popote Ulipo" huku ukisisitiza kuendelea kutoa huduma bora kupitia mifumo ya TEHAMA.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Hadhari,Takwimu na Udhibiti wa Majanga, Bw. Ibrahim Maftah ambaye aliwaongoza wafanyakazi wa makao makuu na wateja katika uzinduzi huo.

Amesema kuwa Wiki ya Huduma kwa Wateja ilianzishwa rasmi kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja na juhudi za wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wateja. "Kwa sasa Mfuko umekamilisha taratibu zote za ufunguzi na ulipaji wa mafao kupitia mtandao na hivyo kutoa fursa kwa wanachama waliopo mbali na ofisi kuweza kufungua madai huko huko waliko, kufuatilia maendeleo ya ulipaji na hatimaye kulipwa kwa mujibu wa kanuni za ulipaji wa mafao," amesema.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Marko Masaya
amesema maadhimisho hayo yanafanyika ofisi zote za mikoa na yanatoa nafasi kwa watumishi na wateja kuungana pamoja kuadhimisha wiki hii.

Akitoa neno la shukrani Meneja Mafao wa NSSF, Bw James Oigo amesema watumishi wa Mfuko wataendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje.