News
WATUMISHI NSSF WASHIRIKI BUNGE BONANZA
.jpeg)
Baadhi ya Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), tarehe 1 Februari, 2025 wameshiriki mazoezi ya pamoja kwenye Tamasha la Michezo la Bunge Bonanza, lililofanyika Viwanja vya John Merlin Sekondari, Jijini Dodoma.
Akizungumza katika bonanza hilo, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF, Bi. Ritha Nguruwe, amesema wameshiriki tamasha hilo kwa sababu mazoezi ni muhimu kwa watumishi na yanawasaidia kuwaepusha na magonjwa yasiyo yakuambukiza.
“NSSF tumeshiriki katika bonanza la Azania Bunge Bonanza lengo ni kuendelea kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi kwa sababu ni muhimu kwa afya hasa watumishi ambao muda mwingi kazi zetu tunazifanya tukiwa tumekaa,”alisema Bi. Ritha.