emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

WAZIRI SANGU APONGEZA UBUNIFU WA NSSF AKITEMBELEA MABANDA YA MAONESHO


Ni katika kuelekea Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii *Pia Uzinduzi wa Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri 'Hifadhi Scheme' Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, kabla ya kuzindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri 'Hifadhi Scheme' Mhe. Sangu alipongeza NSSF kwa maandalizi makubwa waliyoyafanya katika maonesho hayo, na kusisitiza kuwa Hifadhi Scheme inaonesha namna ambavyo Serikali inavyowajali wananchi wote hususan waliojiajiri. Awali, akitoa taarifa kwa Waziri Sangu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, alieleza umuhimu wa hifadhi jamii kwa wananchi waliojiajiri ambao ndio sehemu kubwa ya Watanzania.