News
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NSSF SONGWE

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2025 katika Mkoa wa Songwe, ikiwa na kaulimbiu isemayo “Kidijitali Tumeweza.”
Uzinduzi huo umeongozwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Songwe Bw. William Baruti, ambaye aliwaongoza Wafanyakazi wa Mfuko na Wateja katika maadhimisho hayo yaliyolenga kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa njia za kidijitali na kuongeza huduma karibu na wanachama.