News
CHANGAMKIENI FURSA KUJIUNGA NA KUCHANGIA NSSF

Hayo yalisemwa tarehe 28 Julai, 2024 na Afisa Mwandamizi wa Sekta Isiyo Rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Donald Maganga, wakati akitoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa UWKMT, Dayosis ya Mashariki, ambapo aliwaeleza umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Bw. Maganga amesema NSSF imeweka utaratibu mzuri wa kila mwananchi kujiunga na kuchangia NSSF, ambapo kwa mwezi kima cha chini cha kujiwekea akiba ni shilingi 30,000. Amesema NSSF imeweka mifumo rafiki na rahisi ya TEHAMA ambayo inamrahisishia mwanachama kuwasilisha michango na kuangalia taarifa zake mbalimbali kupitia simu ya kiganjani bila ya kulazimika kufika katika ofisi za Mfuko.
Bw. Maganga amesema mwanachama baada ya kujiunga na kuanza kuchangia atanufaika na faifa mbalimbali ikiwemo mafao ya muda mrefu na muda mfupi likiwemo la matibabu.