News
HIFADHI YA JAMII KWA WOTE
Staa wa mchezo ni mwananchi yeyote aliye jiajiri anaweza kujiunga na NSSF kwa ajili ya kujichangia kidogo kidogo kuanzia Tsh 30,000 na kuendelea ili baadaye naye NSSF ije kuwa Staa wa mchezo wake kwa kuwa na uzee uliobora kwa kupata Mafao, Mwanachama akichangia miezi 3 anaanza kupata fao la matibabu bure, lakini anatakiwa awe anachangia kila mwezi TZS 30,000 kwa mtu mmoja au 52200 kwa Mke/Mume na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18 au 21 kama wanasoma.
Namna ya kujiunga kupitia mitandao ya simu;
1. Piga *152*00#
2. Bonyeza 3 Ajira na Utambuzi
3. Bonyeza 6 NSSF
4. Bonyeza 1 Jisajili kisha fuata maelekezo
Namna ya kuchangia kupitia mitandao ya simu;
1. Piga *152*00#
2. Bonyeza 3 Ajira na Utambuzi
3. Bonyeza 6 NSSF
4. Bonyeza 2 malipo
5. Bonyeza 2 mwanachama kisha fuata maelekezo

