emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

KUELEKEA SIKU YA UKIMWI DUNIANI 2023*NSSF kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWIWafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hiafdhi ya Jamii (NSSF) wakitoa elimu ya hifadhi jamii kwa wanachama na wananchi waliotembelea banda la Mfuko kwenye maonesho ya kuelekea siku ya UKIMWI duniani yanayoendelea katika Uwanja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Morogoro mkoani Morogoro.Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2023 yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Jamii iongeze kutokomeza UKIMWI”. NSSF pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao pia inatekeleza Mwongozo wa kudhibiti VVU/UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi kwa kutumia waelimishaji rika mahala pa kazi kwa kutoa elimu jinsi ya kujikinga na maambukizi ili kulinda nguvu kazi kwa manufaa ya NSSF, wanachama na Taifa kwa ujumla.