emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

MSTAAFU AFUNGUKA MAZITO ASEMA BILA YA NSSF ANGEADHIRIKA






Mzee Anselmi Fungosita ambaye ni mwanachama mstaafu wa NSSF, ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuendelea kumlipa pensheni yake ya uzee kila mwezi kwa kipindi cha miaka kumi na nne (14) sasa bila ya kupata usumbufu wowote na kuendelea kuishi maisha mazuri.




Mzee Fungosita amesema hayo mjini Morogoro wakati alipotembelea banda la NSSF katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSH) yanayoendelea katika viwanja vya Tumbaku.




“Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa uhai huu na kuifanya Serikali yetu ya Tanzania kuweka Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii kama NSSF, kwa sababu mimi nimestaasfu miaka kumi nne iliyopita na nilivyoenda katika ofisi za NSSF nilikutana na wafanyakazi ambao walinishauri vizuri, waliniambia baba usichukue fedha zako zote chukua kiasi fulani na kilichobaki utakuwa unapokea pensheni ya uzee kila mwezi. Nilikubali ndio maana mpaka leo hii nina faidi matunda kwa kupata malipo yangu ya pensheni kila mwezi ambayo yana nisaidia kupata mahitaji yangu,” alisema Mzee Fungosita.




Aidha aliupongeza Mfuko kwa kuweza kuyafikia makundi mbalimbali ya wajasiriamali na kuwapa elimu ili waweze kujiunga na kuchangia katika Mfuko kwa ajili ya maisha yao baadaye.




“NSSF mmefanya kitu kizuri sana ninawapongeza kwa kutoa fursa kwa watu waliojiajiri wenyewe ili waweze kunufaika na hifadhi ya jamii ikiwemo mafao ya uzee," amesema.




Amebainisha kuwa, bila ya pensheni anayolipwa na Mfuko maisha yake yangekuwa magumu hasa ukizingatia kuwa hana nguvu za uzalishaji mali.



Katika hatua nyingine, Mzee Fungosita ambaye ni mwanachama mstaafu wa NSSF amesema kuwa NSSF inampa fursa mbalimbali ikiwemo kupata mkopo benki kupitia pensheni yake.



“NSSF ndio familia yangu hilo siwezi kupinga kwa sababu mimi leo sina kazi nilishastaafu miaka kumi na nne iliyopita, lakini NSSF inanilipa mafao yangu kila mwezi bila ya kuchelewa," amesema.