emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

Naibu Waziri Dkt.Evaline apongeza Mafanikio ya NSSF


Naibu Waziri Dkt.Evaline apongeza Mafanikio ya NSSF Na Mwandishi Wetu, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi, ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mafanikio yaliyopatikana, hususan katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, akibainisha kuwa Mfuko huo umekua kwa kasi na kuendelea kupata hati safi. Dkt. Evaline alitoa pongezi hizo Mei 18, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za NSSF jijini Dar es Salaam. “Naomba niwapongeze kwa hatua mlizofikia tangu kuanza kwa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita. Mfuko umeonyesha mafanikio makubwa, hususan katika ongezeko la wanachama, ukusanyaji wa michango, uwekezaji na ulipaji wa mafao,” alisema. Alibainisha kuwa uwekezaji wa NSSF unaendelea kuwa na mchango chanya kwa uchumi wa Taifa kwa kuchochea ajira na kuboresha vipato vya wananchi. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuhamasisha wananchi wengi zaidi, hususan waliojiajiri, kujiunga na NSSF ili kunufaika na mafao mbalimbali, yakiwemo ya matibabu. Sambamba na hayo, alieleza kuwa NSSF imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono ajenda ya nishati safi kupitia usambazaji wa mitungi ya gesi, hatua inayolenga kulinda afya za wananchi na mazingira. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, alimshukuru Naibu Waziri kwa ziara hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu. Alisema Mfuko utaendelea kuboresha huduma na kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya wanachama na taifa kwa ujumla.