emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NAIBU WAZIRI MKUU ALIPOTEMBELEA BANDA LA NSSF NA KUJIONEA HUDUMA ZINAZOTOLEWA


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameupongongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuendelea kufanya kazi nzuri katika uwekezaji pamoja na kutoa huduma kwa wanachama. Mhe. Dkt. Biteko amesema hayo alipotembelea banda la NSSF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani katika viwanja vya General Tyre, Njiro Jijini Arusha.


Awali, akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mashomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF, Bi. Lulu Mengele alimueleza mgeni rasmi huyo kuwa Mfuko unatekeleza majukumu makuu manne ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao. Amesema mpaka sasa thamani ya Mfuko imefikia Trioni 8.1 na kuongeza kuwa ongezeko hilo linatokana na uongozi mzuri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.