News
NSSF SIMIYU YAHUDUMIA WANANCHI WIKI SHERIA

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Simiyu, unaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Sheria, yanayoendelea katika katika Viwanja vya CCM Simiyu.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenan Kihongosi, alitembelea Banda la NSSF na kujionea wananchi wanavyopata huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko. Kupitia maadhimisho hayo NSSF inatoa msaada wa kisheria kuhusu mafao na michango, kuandikisha wanachama wapya, kutatua kero mbalimbali za wanachama pamoja na huduma za digitali.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050: Nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”.