emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF YASHIRIKI KITAIFA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI– MEI MOSI 2026


NSSF YASHIRIKI KITAIFA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI– MEI MOSI 2026 Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeungana na wafanyakazi kutoka taasisi na mashirika mbalimbali nchini kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Mei, ambapo kaulimbiu ya mwaka 2026 ni “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.” NSSF imeshiriki katika maadhimisho hayo kitaifa yaliyofanyika mkoani Njombe, yakiongozwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika maadhimisho hayo Kitaifa, Mfuko uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba. Sambamba na ushiriki huo wa kitaifa, NSSF pia ilishiriki maadhimisho hayo katika ngazi za mikoa kupitia ofisi zake nchi nzima. NSSF inaendelea kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma ili kuchangia maendeleo ya taifa. #MeiMosi2026 #NSSF #Wafanyakazi #Tanzania