emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA WACHIMBAJI MADINI MBEYA*Meneja wa NSSF Mbeya aainisha umuhimu wa kujiunga na kuchangia NSSF

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mbeya leo tarehe 22 Nov,2022 umeshiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Mbeya (MBEREMA) uliofanyika katika ukumbi wa Omary City Hotel Wilaya ya Chunya.

Ambapo Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya,Deus Jandwa alitumia fursa hiyo kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa washiriki wa mkutano huo juu ya sheria ya NSSF, majukumu, huduma pamoja na Mafao yanayotolewa na NSSF.

Pia,alitoa wito kwa wadau wa madini wa Mkoa huo na nchi nzima kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kujiunga na kuchangia NSSF ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko ili kujenga kesho iliyo njema.