emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YAWAHAMASISHA WAAJIRI KUCHANGAMKIA MSAMAHA WA TOZO



Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Omary Mziya, amewahimiza waajiri nchini kutumia fursa ya msamaha wa tozo unaoendelea hadi Desemba 2026 kwa kulipa madeni ya michango, huku akiwasisitiza wananchi waliojiajiri kujiunga na Mfuko kupitia Skimu ya Hifadhi ili kunufaika na mafao yanayotolewa.

Bw. Mziya ametoa wito huo alipotembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba), ambapo alijionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko kwa wanachama, waajiri na wananchi.

Amesema NSSF inaendelea kupanua wigo wa hifadhi ya jamii kwa kuwafikia wananchi waliojiajiri, huku akiwasihi waajiri kuwaandikisha wafanyakazi wao, kuwasilisha michango kwa wakati na kutumia kikamilifu fursa ya msamaha kwa kulipa michango yao.

Aidha, ameongeza kuwa NSSF imeendelea kuboresha huduma zake kwa njia ya kidijitali, hivyo wanachama na waajiri wanaweza kupata huduma kwa urahisi popote walipo bila kulazimika kufika katika ofisi za Mfuko.

#NSSF #SabaSaba2026 #SkimuYaHifadhi #HifadhiYaJamii #MsamahaWaTozo #HudumaKidijitali