emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

WAFANYAKAZI WANAWAKE WA NSSF MKOA WA NJOMBE WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026


Wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Njombe wameungana na wenzao kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani 2026. Maadhimisho hayo yamefanyika kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii na sehemu za kazi, huku yakibeba kauli mbiu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira ya 2050.”