emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

Waziri Sangu atembelea banda la NSSF katika kilele cha Maonesho ya Wiki ya Usalama Mahala pa kazi 2026 (OSHA) Mkoani Njombe


Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Mahala pa kazi 2026 (OSHA) yaliongozwa na kauli mbiu isemayo “Mazingira Bora ya Kisaikolojia na Kijamii Kazini ni Njia ya Kuhimarisha Ustawi na Wafanyakazi na Kujenga Taasisi Imara” Kauli mbiu hiyo imelenga kuhamasisha waajiri na wafanyakazi kuzingatia si tu usalama wa kimwili na mazingira ya kazi bali pia afya ya akili na ustawi wa kijamii mahali pa kazi. NSSF imeshiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo kuhusu mafao, uandikishaji wa wanachama wapya, hususan kutoka sekta binafsi na kwa wananchi waliojiajiri, njia rahisi za kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za kidigitali, ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na kuhamasisha wanachama kutumia mifumo ya kidijitali ya Mfuko, ili kupata huduma mbalimbali kama vile taarifa za michango, kutengeneza kumbukumbu za namba za malipo (Control number), kulipia michango na kufungua madai.