emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NSSF MTWARA


Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2025 katika Mkoa wa Mtwara ikiwa na kaulimbiu isemayo “Kidijitali Tumeweza.” Uzinduzi huo umeongozwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Mtwara Bw. rebule Maira, ambaye aliwaongoza Wafanyakazi wa Mfuko na Wateja katika maadhimisho hayo yaliyolenga kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa njia za kidijitali na kuongeza huduma karibu na wanachama.