News
HUDUMA ZA NSSF KIDIJITALI ZAWAVUTIA WANACHAMA SABASABA

NSSF inazidi kuboresha huduma kwa wanachama wake kwa kuleta huduma za kidijitali, ambapo sasa mwanachama anaweza kupata huduma muhimu za NSSF kiganjani popote ulipo. Hii ni hatua kubwa katika kuboresha na kurahisisha huduma kwa wananchi wengi zaidi.
Huduma Kiganjani
Wanachama sasa wanaweza kufurahia huduma za NSSF kwa njia ya mtandao, ambapo kupitia simu ya kiganjani mwanachama anapata taarifa zake mbalimbali popote alipo bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.
Ukiwa kwenye banda la NSSF Sabasaba, utaunganishwa moja kwa moja na huduma za kidijitali. Ni rahisi, haraka, na salama!