News
WAFANYAKAZI WANAWAKE WA NSSF SHINYANGA NA KAHAMA WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026
Wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kahama na Shinyanga wameungana na wenzao kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani 2026.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii na sehemu za kazi, huku yakibeba kauli mbiu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira ya 2050.”

