News
MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
.jpeg)
*NSSF inavyoshiriki na kutoa huduma za hifadhi ya jamii nchini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametembelea mabanda ya Taasisi za Umma katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma na kupata maelezo ya utendaji kazi wa Taasisi hizo.
Akiwa katika mabanda hayo, Waziri Simbachawene amewataka watumishi wa Taasisi hizo kuendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuwatumikia wananchi.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) upo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Katika maonesho hayo, NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili kwa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri wenyewe, pia wanapewa elimu jinsi wanavyoweza kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, elimu kuhusu huduma za kidijiti (NSSF Portal).
Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikani”.