News
NSSF YAIBUKA MSHINDI MPIRA WA WAVU, YAIFUNGA TIMU YA BUNGE KATIKA BONANZA LA CRDB BUNGE GRAND BONANZA 2025

Timu ya Mpira wa Wavu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeibuka mshindi dhidi ya timu ya Bunge katika michezo ya CRDB Bank Bunge Grand Bonanza 2025.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Katika bonanza hilo, Wafanyakazi wa NSSF waliongonzwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Bw. Yahya Mudhihiri na kushiriki kikamilifu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule pamoja na Mbunge wa Mchinga, Mhe. Salma Kikwete waliwapongeza wachezaji wa NSSF walioshiriki bonanza hilo.
Ushiriki wa NSSF katika bonanza hilo unaakisi dhamira ya Mfuko kuendeleza afya, mshikamano na mahusiano ya kijamii kwa njia ya michezo, huku ikiimarisha ushirikiano baina ya taasisi na wadau mbalimbali.