News
MKURUGENZI MKUU WA NSSF AWAHUDUMIA WANANCHAMA NA WANANCHI SABASABA
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, akiendelea kuwahudumia wanachama na wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma za hifadhi ya jamii alipotembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Karibu Banda Na. 13 upate huduma za NSSF, ujiandikishe uanachama, upate elimu kuhusu hifadhi ya jamii, elimu kuhusu mafao na huduma mbalimbali, pamoja na taarifa kuhusu huduma za NSSF kidijitali.
NSSF – Huduma Bora, Kipaumbele Chetu.

