emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF KATIKA WIKI YA HUDUMA YA SHERIA




Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unashiriki na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Sheria, yaliyoanza tarehe 24 mpaka 30, Januari, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.



Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NSSF, Suleiman Msangi ametembelea maadhimisho hayo na kumuhudumia mwanachama aliyefika kupata huduma katika banda la NSSF.



Kupitia Maadhimisho hayo, NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii, msaada wa kisheria, kuandikisha wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyorasmi, kutatua kero mbalimbali za wanachama pamoja na huduma za digitali.



Maadhimisho hayo yalianza tarehe 24 Januari na yatamalizika tarehe 30, Januari, 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo "UMUHIMU WA DHAMANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA: NAFASI YA MAHAKAMA NA WADAU KATIKA KUBORESHA MFUMO JUMUISHI WA HAKI JINAI"

uchaguzi