emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

MWENYEKITI WA BODI YA NSSF ARIDHISHWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANACHAMA SABASABA


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Mwamini Malemi, amejionea namna ambavyo wanachama na wananchi wanavyohudumiwa kwa weledi na ufanisi katika banda la NSSF kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Bi. Malemi ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waliojiajiri kujiunga na kujiwekea akiba ili wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF yakiwemo ya matibabu.

Aidha, ametembelea mabanda ya kampuni tanzu za NSSF, Mkulazi inayozalisha sukari, na Sisalana inayozalisha bidhaa za katani ambazo ni sehemu ya uwekezaji wa kimkakati wa Mfuko katika kukuza uchumi na kuimarisha mafao kwa wanachama.