emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

MKURUGENZI MKUU WA NSSF AJIONEA NAMNA WANACHAMA WANAVYOHUDUMIWA KWA UFANISI SABASABA


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, na kushuhudia namna wanachama na wananchi wanavyohudumiwa kwa ufanisi na weledi.

Bw. Mshomba amejionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko, zikiwemo elimu ya hifadhi ya jamii, usajili wa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, pamoja na utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya mifumo ya kidijitali kama NSSF Portal na NSSF App. Vilevile, amejionea namna NSSF inavyotoa taarifa kuhusu miradi yake ya uwekezaji wa nyumba na viwanja.