emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF, TUICO WASAINI MIKATABA YA MUUNDO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI NA BARAZA LA MAJADILIANO



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), wamesaini mikataba ya muundo wa Baraza la Wafanyakazi na Baraza la Majadiliano. Kwa upande wa NSSF mikataba hiyo imesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba na kwa upande wa TUICO umesainiwa na Bw. Victor Kom, Katibu Msaidizi wa Sekta ya Fedha, hafla hiyo ya uwekaji saini ilifanyika katika Ofisi za NSSF zilizopo jengo la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.