emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA DODOMA, YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII NA KUSAJILI WANACHAMA WAPYA


NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA DODOMA, YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII NA KUSAJILI WANACHAMA WAPYA

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unashiriki katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, ambapo unaendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii na kusajili wanachama wapya.

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 1 Agosti 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Akifungua maonesho hayo, Dkt. Nchemba alisisitiza umuhimu wa kuongeza tija katika sekta ya kilimo ili kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Aidha, aliwahimiza wakulima kuwekeza katika uzalishaji wenye tija na ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Katika maonesho hayo, NSSF inatoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu kuhusu hifadhi ya jamii, usajili wa wanachama wapya, pamoja na ushauri kuhusu mafao na huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo:

"Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."