News
RAIS SAMIA ATEMBELEA UJENZI WA MRADI WA HOTELI YA KITALII YA NYOTA TANO CAPRIPOINT MWANZA

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza mara baada ya kupokea maelezo kuhusu ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) iliyopo jijini Mwanza, ambapo aliipongeza NSSF kwa mradi wa hoteli hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu taratibu za kupitisha miradi mbalimbali ambayo huanzia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ushauri na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inasimamia sekta ya hifadhi ya jamii. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inawekeza kwa lengo la kulinda thamani ya michango ya wanachama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF) Masha Mshomba, akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo jijini Mwanza, ambapo alisema ujenzi huo unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Juni 2024 baada ya kupatikana muendeshaji wa hoteli mwishoni mwa mwezi huu.
Meneja Usimamizi wa Miradi NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania namna mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano utakavyokuwa. Mradi huo una ghorofa 16, vyumba 168 vya kulala vya aina mbalimbali ikijumuisha sehemu ya kupumzikia Rais (Presidential Suite), migahawa, sehemu za vinywaji na michezo (sports bar).
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.