News
Wananchi Wajitokeza Kwa Wingi Banda la NSSF Maonesho ya 8 ya Madini Geita

Wananchi wengi wamejitokeza kupata elimu ya hifadhi ya jamii katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwenye Maonesho ya 8 ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Kupitia maonesho hayo, NSSF inaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuandikishaji wa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, elimu ya mafao yanayotolewa na Mfuko,
uelewa kuhusu mifumo ya TEHAMA na huduma za kidijitali za NSSF na utoaji wa taarifa kuhusu miradi ya uwekezaji ya Mfuko.
Wananchi waliojipatia huduma katika banda hilo wamepongeza jitihada za NSSF za kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii.